NEWS

Thursday, 10 June 2021

Rais Samia amteua Balozi Batilda RC mpya Tabora, atengua uteuzi wa Chalamila, ampeleka Mhandisi Gabriel Mwanza, Hapi ndani ya Mara



Balozi Dkt Batilda Salha Buriani

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya wakuu wa mikoa, ambapo amemteua Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga, Balozi Dkt Batilda Salha Buriani kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

Taarifa iliyotolewa leo Juni 11, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais - Ikulu, Jaffar Haniu, imesema Rais Samia ametengua uteuzi wa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Albert Chalamila na kumhamisha Mkuu wa Mkoa wa Mara, Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi kwenda Mwanza.


Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Rais Samia pia amemhamisha Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Ally Salum Hapi kwenda Mkoa wa Mara - kuziba nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Gabriel aliyehamishiwa Mwanza.


Ally Salum Hapi

Aidha, Rais Samia amemteua Katibu Tawala wa Wilaya ya Simanjiro, Zuwena Omari Jiri kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga - kuchukua nafasi ya Balozi Dkt Batilda aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages