NEWS

Tuesday 29 June 2021

RUWASA Tarime yazituza Jumuiya za watumia maji
WAKALA wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Wilaya ya Tarime mkoani Mara, imegawa zawadi za vyeti na fedha taslimu kwa jumuia tatu za watumia maji zilizofanya vizuri katika usimamizi na uendeshaji wa miradi ya maji wilayani humo.

Jumuiya hizo na zawadi zake zikiwa kwenye mabano ni Nyamwaga - Keisangora (cheti na Sh 100,000), Kewanja (cheti na Sh 60,000) na Gamasara (cheti na Sh 40,000).Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote amekabidhi zawadi hizo kwa jumuiya hizo, wakati wa mkutano wa wadau wa maji mjini Tarime, leo Juni 29, 2021.

Mkutano huo umefunguliwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Tarime, John Marwa ambaye ametumia nafasi hiyo kuwataka wananchi kufichua wahujumu wa miundombinu ya maji ili wachukuliwe hatua za kisheria.(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages