
Mwenyekiti wa Kurya Social Group, CPA James Magoti (aliyekaa katikati), akiongoza Mkutano Mkuu wa KSG uliofanyika mjini Tarime jana. Kushoto kwake ni Katibu wa KSG, Fred Mariba na wa kwanza kulia ni Mhasibu wa KSG, Mugini Phanuel.
Uongozi wa Kurya Social Group (KSG) umemteua mwanahabari Mugini Jacob kuongoza kamati maalum itachayokata na kubuni mradi wa kiuchumi wa KSG.
Kamati hiyo ilitangazwa Jumapli, Desemba 28, 2025 katika Mkutano Mkuu wa KSG uliofanyika kwenye Hoteli ya NK mjini Tarime, mkoani Mara.
Mwenyekiti wa KSG, CPA Lucas Magoti, alimtaangza Mugini kuwa ataongoza kamati hiyo akisaidiwa na wajumbe wengine saba, wakiwemo wabobezi wa wa fani mbalimbali, ikiwemo sheria na masuala ya uchumi na jamii.

Mugini ambaye kitaaluma ni mwanahabari, Mkurugenzi wa Mara Online na Mhariri Mtendaji (ME) wa Gazeti la Sauti ya Mara, amepata mafunzo ya habari na mawasiliano ya umma ndani na ya nchi.
Kwa sasa, Mugini pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari Mkoa wa Mara (MRPC) na Mweka Hazina wa Umoja wa Kuwezesha Waandishi wa Habari (Reporters Empowerment Union - REU).
Aidha, CPA Magoti alisema Katibu wa kamati hiyo atakuwa Justa Magabe ambaye ni Diwani wa Kata ya Nyakonga na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini).

Wanachama wa KSG wakifurahia picha ya pomoja baada ya Mkutano Mkuu wa 2025
“Kamati hii malaam ya kuchakata mradi wa kiuchumi ambao tutaanzishwa, Mweyekiti wake atakuwa Mugini Jacob na Katibu wake atakuwa Mhe. Justa Magabe,” Mwenyekiti wa KSG, Magoti, alisema na kuongeza kuwa anataka kuona KSG inakuwa na mageuzi makubwa ya kiuchumi na kuendelea kugusa wahitaji na kuenzi mila na desturi nzuri kwa ustawi wa jamii.
Alitangaza wajumbe wengine wa kamati hiyo kuwa ni Dkt. Justine Chacha, Diwani Joseph Goryo, David Gichogo, Elia Marwa, Marwa Charles na Marwa Stephen.

Kamati hiyo imepewa muda wa miezi mitatu kukamilisha kazi yake.
Wakati huo huo, CPA Magoti aliipongeza Mara Online kwa kubuni na kutengeza logo (nembo) ya KSG.
“Hii logo yetu ni nzuri na imebuniwa na kutengenezwa na Mara Online. Tunamshukuru Mkurugenzi wa Mara Nline, Mugini, kwa mchango huu wa logo ambao hauwezi kusahaulika,” CPA Magoto aliema wakati akifungua mkutao huo ambao pia ulipambwa na ngoma ya Lirandi ya jamii ya Wakurya.

Mkutano ukiendelea
KSG ina wanachama ambao ni wazaliwa wa Tarime wanaoishi na kufanya kazi katika maeneo mbalimbali nchini, na umoja huo umejikita katika kuendeleza ustawi wa jamii.
No comments:
Post a Comment