NEWS

Monday 28 June 2021

TRA yahamasisha ulipaji kodi mlango kwa mlango
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) imeanza kampeni maalum ya mlango kwa mlango - kuhamasisha wadau kulipa kodi kwa wakati ili kuepuka msongamano katika tarehe za mwisho wa mwezi.

Akizungumza wakati wa kuendesha kampeni hiyo wilayani Tarime leo Juni 28, 2021, Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi Mwandamizi wa TRA Mkoa wa Mara, Zake Wilbard Rwiza (pichani juu) amesema kulipa kodi mapema kunamwepushia mdau adhabu na faini zisizo za lazima.

“Ni bora kulipa kodi kwa wakati, kwa sababu kodi ni sehemu tu ya faida iliyochujwa, na adhabu na faini ni sawa na virusi kwenye biashara za wadau wa kodi,” amesema Rwiza.

Ametaja vyanzo vya kodi ya serikali kuwa ni pamoja na kodi kwenye mishahara kwa waajiriwa, sehemu ya faida kwa wafanyabiashara na sehemu ya pato kwenye uwekezaji (Return on Investment – ROI).

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages