NEWS

Monday 12 July 2021

DC Chikoka aweka wazi dira yake Rorya




MKUU mpya wa Wilaya ya Rorya, Juma Issa Chikoka - maarufu kama Chopa Mchopanga, ametuma ujumbe kwa wananchi wilayani humo, kwamba wategemee kuona kiongozi [akimaanisha yeye] mwenye dira angavu ya kutatua changamoto zao za kisekta.

“Wananchi wa Rorya wategemee kupata ushirikiano wa kuridhisha kutoka kwangu, katika kutatua changamoto zao zikiwemo za afya, elimu, maji na miundombinu ya barabara,” Chikoka amesisitiza katika mahojiano maalum na Mara Online News ofisini kwake, wiki iliyopita.

Sambamba na hilo, amesema atakuwa mtumishi na kiongozi anayependa kuona wana-Rorya wakifanya kazi kwa bidii na kutimiza wajibu wao katika kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa manufaa yao, wilaya na Taifa.


DC Chikoka akifafanua jambo wakati wa mazungumzo hayo

Kuhusu uvuvi, DC huyo amesema ataelekeza nguvu kubwa katika kushawishi wawekezaji kwenye sekta hiyo, kwa lengo la kuinua uchumi wa wavuvi, pato la wilaya na Taifa.

“Asilimia 77 ya eneo la Rorya ni ziwa [Ziwa Victori], hivyo ninataka kuona ziwa hili linawanufaisha wananchi wa wilaya hii kiuchumi, tuwawezeshe kufanya uvuvi wa kisasa na wenye tija, ili kupaisha pato lao, la wilaya na Taifa.

“Wakati huo huo, wananchi waache vitendo vya uvuvi haramu, kwa sababu ni risk (hatari) kwao na vinasababisha upotevu wa mapato ya serikali,” amesema Chikoka na kuahidi kuendelea kueleza alivyojipanga kutatua changamoto za sekta nyingine wilayani Rorya.

(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages