NEWS

Tuesday 27 July 2021

DC Mashinji atamani utalii uongoze kuchangia maendeleo wilayani Serengeti
MKUU wa Wilaya (DC) ya Serengeti mkoani Mara, Dkt Vicent Mashinji (pichani juu), ametaja moja ya mipango ya maendeleo atakayoipa kipaumbele kuwa ni pamoja na kuhakikisha wilaya hiyo inakuwa kitovu cha mapumziko ya watalii kabla ya kuingia na mara wanapotoka kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Akizungumza katika kikao na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti mjini Mugumu hivi karibuni, Dkt Mashinji amesema eneo kubwa la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti lipo ndani ya wilaya hiyo, hivyo inapaswa kuongoza kwa upatikanaji wa huduma zinazohitajika kwa watalii, ili kuchochea maendeleo yake.

Pamoja na mipango ya ujenzi wa uwanja wa ndege na hoteli za kitalii, DC Mashinji amesema wanajipanga pia kujenga viwanja vya michezo vitakavyoshawishi wanamichezo wa kimataifa kuchagua wilaya hiyo kama sehemu yao nzuri ya kutembelea kwa ajili ya kupumzika na kufanya mazoezi.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages