NEWS

Thursday 22 July 2021

DC Tarime, Mara Online wateta maandalizi safari ya kuwapokea nyumbu Serengeti



Mhariri Mtendaji wa Blogu ya Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara, Jacob Mugini (kushoto) akimkabidhi Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mtenjele nakala ya toleo la wiki hii la gazeti hilo - wakati alipomtembelea DC huyo ofisini kwake leo Julai 22, 2021, kwa ajili ya mazungumzo maalum kuhusu maandalizi ya safari ya wakazi wa Tarime kwenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango jipya la Lamai lililopo kijijini Karakatonga, itakayofanyika Julai 25, 2021. Kaulimbiu ya hamasa ya safari hiyo inasema “Wanyamapori Wetu, Utalii Wetu”.

  

 Safari hiyo inaratibiwa na hifadhi hiyo kwa kushirikiana na taasisi ya Mara Online na Goldland Hotel and Tours. Tayari wananchi wengi wamejitokeza kununua tiketi kwa ajili ya safari hiyo, iliyopewa jina la "kuwapokea nyumbu Serengeti".

 

Mugini ambaye pia ni Afisa Habari wa Taasisi ya Kizalendo Tanzania (TPO) Mkoa wa Mara, amemweleza DC Mtenjele kwamba maandalizi ya safari hiyo yamekamilika kwa asilimia 90.

 

TPO Wilaya ya Tarime, chini ya Mwenyekiti wake, Philipo Lusotola imeshiriki kuhamasisha safari hiyo ya utalii wa ndani.

 

MaraOnlineNews-Updates

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages