
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (kulia), akikaribishwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara, Kanali Evans Mtambi (katikati), alipowasili kutembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa, mjini Musoma jana.
Na Mwandishi Wetu
Musoma
------------
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, ameahidi kushirikiana na viongozi wengine wakiwemo wabunge wa mkoani Mara kufuatilia utekelezaji wa miradi ya kimkakati ya mkoa huo iliyoainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2025-2030.
Ametaja miradi ya kimkakati itakayotekelezwa mkoani Mara kuwa ni pamoja na reli ya kutoka Tanga, Arusha hadi Musoma, ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa Serengeti, barabara ya lami inayounganisha mikoa ya Arusha na Mara, na barabara zinazounganisha wilaya za mkoa wa Mara.
Waziri Nyansaho aliyasema hayo Jumapili, Desemba 21, 2025 alipofanya ziara wilayani Musoma na kutembelea ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) leo tarehe 21 Disemba, 2025.

Hiyo ni ziara ya kwanza kwa Dkt. Nyansaho ambaye ni mwenyeji wa wilaya ya Serengeti na mdau mkubwa wa maendeleo kutembelea mkoa wa Mara, tangu alipoteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwa Mbunge na baadaye Waziri.
No comments:
Post a Comment