NEWS

Friday 30 July 2021

TANZIA: DKT WINANI AFARIKI DUNIA, WENGI WAMLILIADkt Hudson Winani enzi za uhai wake

MWASISI na Mkurugenzi wa Tarime Good Will Foundation (TGF), inayoendesha moja ya hospitali maarufu katika mji wa Tarime mkoani Mara, Dkt Hudson Winani (84) amefariki dunia, mtoto wake, Hezron Winani amethibitisha.

“Mzee amefariki dunia leo alfraji (saa 11) na tupo kwenye vikao kwa ajili ya mipango ya mazishi,” Hezron ameimbia Mara Online News kwa njia ya simu leo Julai 30, 2021 kutoka jijiji Mwanza.

Dkt Winani (katikati) enzi za uhai wake

Hezron amesema Dkt Winani amekutwa na mauti akiwa kwenye matibabu katika hospitali ya Hurumia Watoto ya jijini Mwanza, na kwamba mazishi ya marehemu yanatarajiwa kufanyika Jumatano ijayo.

Wananchi mbalimbali wameeleza kushtushwa na kifo cha Dkt Winani, wakimuelezea kama mtu aliyetumia taaluma yake ya udaktari kuhudumia watu bila kubagua wenye nacho na wasionacho.
Dkt Winani (kushoto) kazini enzi za uhai wake

“Kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Dkt Hudson Winani kilichotokea Mwanza,” Mchungaji wa Kanisa la SDA Tarime Central, Deogratias Nyangibo ameandika kwenye group la WhatsApp la kanisa hilo leo.

Mara Online News itaendelea kuwajuza wasomaji maendeleo ya taratibu na mipango ya mazishi ya Dkt Winani.

MaraOnlineNews-Updates

1 comment:

  1. Rest in peace Winani you worked kindly to save lives

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages