NEWS

Tuesday 6 July 2021

Frida Mwera, wengine 6 wateuliwa na Waziri kuwa wajumbe wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala
FRIDA Peter Mwera (pichani juu) ameteuliwa kuwa Mjumbe wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, chini ya Mwenyekiti wa baraza hilo, Profesa Hamis Masanja Malebo aliyeteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan, hivi karibuni.

Frida ambaye ni mtumishi katika Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ameteuliwa kushika nafasi hiyo pamoja na wajumbe wengine sita walioteuliwa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Dorothy Gwajima.

Wajumbe wengine walioteuliwa ni Saada Ahmed Saum, John Kabadi Lupima, Khalid Kibinda, Simon Emmanuel Rusigwa, Elizabeth Lema na Salome Protas.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa umma hivi karibuni na Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Catherine Sungiura, uteuzi wa wajumbe hao umeanza Julai 3, 2021.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages