
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (aliyesimama), akizungumza katika kikao cha pamoja cha viongozi wakuu wa wizara hiyo walipokutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, leo Januari 6, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho (wa pili kushoto), Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka (wa kwanza kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe (kulia) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania Jenerali Jacob John Mkunda (wa pili kulia), mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar leo Januari 6, 2026.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Dkt. Samia Suluhu Hassan, akiwa kwenye picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Simeon Nyansaho, Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi Dkt. Moses Kusiluka, Katibu Mkuu Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Faraji Mnyepe, Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Jacob John Mkunda na Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa, Meja Jenerali Rajabu Mabele, miongoni mwa maafisa wengine wa jeshi mara baada ya mazungumzo yaliyofanyika Ikulu ndogo ya Tunguu, Zanzibar, leo Januari 6, 2026. (Picha zote na Ikulu)
No comments:
Post a Comment