NEWS

Tuesday 27 July 2021

Utalii wa ndani Hifadhi ya Serengeti: Mara Online yaweka alama



MHARIRI Mtendaji wa Mara Online News, Jacob Mugini (katikati) akionesha zawadi maalumu yenye Bendera ya Taifa la Tanzania, aliyotunukiwa na Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi na Maendeleo ya Utalii kutoka Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) Kanda ya Magharibi, Neema Mollel (kushoto mbele), ikiwa ni ishara ya kutambua mchango mkubwa uliooneshwa na chombo hicho cha habari cha kidijitali katika kuhamasisha utalii wa ndani kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti. Wengine ni wahifadhi na baadhi watalii wa ndani kutoka Tarime waliotembelea hifadhi hiyo kupitia lango la Lamai, juzi.

Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Col. Michael Mtenjele naye aliipongeza Mara Online News kwa kuwa mstari wa mbele katika uhamasishaji uliowezesha watalii wa ndani zaidi ya 60 kutoka wilayani humo kutembelea hifadhi hiyo kupitia lango la Lamai, juzi.


Mhariri Mtendaji wa Mara Online News, Jacob Mugini akiwa kazini ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, wakati wa ziara ya watalii wa ndani zaidi ya 60 hifadhini hapo, juzi.


Mhariri Mkuu wa Mara Online News, Christopher Gamaina naye akiwa kazini wakati wa ziara maalumu ya watalii wa ndani kutoka Tarime, katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, juzi.


Baadhi ya watalii wa ndani kutoka wilaya ya Tarime wakifurahia kushuhudia mbashara makundi ya wanyamapori ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, juzi.


Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Col. Michael Mtenjele (katikati) na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Daudi Marwa Ngicho (kushoto) ni miongoni mwa watalii wa ndani zaidi ya 60 kutoka Tarime waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Lamai, juzi. Wanaoonekana nyuma yao ng'ambo ya mto, ni wanyamapori aina ya kiboko.


Afisa Mhifadhi Mkuu na Mkuu wa Kitengo cha Utalii wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tutindaga George (kushoto) akizungumza na watalii wa ndani kutoka wilaya ya Tarime mkoani Mara hifadhini hapo, juzi.


Baadhi ya viongozi wa Taasisi ya Kizalendo Tanzania (TPO) Mkoa wa Mara na Wilaya ya Tarime, wakiwa katika picha ya pamoja na wahifadhi, wakati walipokwenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, juzi.


Sehemu ya makundi ya nyumbu yaliyokuwa kivutio kikubwa kwa watalii wa ndani kutoka wilaya ya Tarime waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, juzi.


Watalii wa ndani kutoka wilaya ya Tarime (waliosimama chini mbele) na watalii wa kigeni (nyuma yao kwenye gari), wakifurahia ubora wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, juzi.

MaraOlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages