NEWS

Tuesday 27 July 2021

Mto Mara: Chachu ya maendeleo ya uhifadhi, utalii Hifadhi ya Serengeti


WANYAMAPORI aina ya kiboko wakifurahia ikolojia ya Mto Mara, Kaskazini mwa hifadhi bora Afrika, yaani Hifadhi ya Taifa ya Serengeti - ambayo ni kivutio cha maelfu ya watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani, kama walivyokutwa na camera ya Mara Online News, juzi.

MKUU wa Wilaya ya Tarime mkoani Mara, Col. Michael Mtenjele (katikati) na Mwenyekiti wa CCM wa Wilaya hiyo, Daudi Marwa Ngicho (kushoto), ni miongoni mwa watalii wa ndani zaidi ya 60 kutoka Tarime, waliotembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kushuhudia mbashara makundi ya wanyamapori mbalimbali, wakiwemo viboko katika Mto Mara, juzi.

Mto Mara ni sehemu muhimu ya ikolojia ya Serengeti, kwani una mchango mkubwa katika uhifadhi wa wanyamapori, wakiwemo nyumbu ambao ni kivutio kikubwa cha utalii kutokana na matukio yao ya kipekee, hususan ya kuvuka mto huo kwenda Mbuga ya Maasai-Mara, kisha kurudi Serengeti kila mwaka.

Mto huo unaanzia kwenye chemichemi za Enopuyapui katika misitu ya Mau nchini Kenya, kisha kupita Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kumwaga maji yake katika Ziwa Victoria, upande wa Tanzania.

MAKUNDI ya nyumbu yakivuka Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

Mbali na uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti, Bonde la Mto Mara lina mchango mkubwa katika ustawi wa maisha ya watu zaidi ya milioni 1.1 katika nchi za Tanzania na Kenya.

Aidha, Mto Mara ni muhimu kwa shughuli mbalimbali za binadamu, zikiwemo za kilimo cha umwagiliaji, maji kwa ajili matumizi ya nyumbani, mifugo na uvuvi. Lakini pia, mto huo unachangia kuimarisha uhusiano kati ya Tanzania na Kenya, kupitia maadhimisho ya Siku ya Mara, inayoadhimishwa Septemba 15 kila mwaka.

Eneo la Bonde la Mto Mara lina ukubwa wa kilomita za mraba 13,325, huku mto wenyewe ukiwa na urefu wa kilomita 400.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages