NEWS

Thursday, 15 July 2021

RC Hapi kazini, akagua mradi wa maji Shirati




MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Ally Salum Hapi (katikati), leo Julai 15, 2021 ametembelea na kukagua mradi wa maji Safi na salama wa mji mdogo wa Shirati wilayani Rorya, unaotekelezwa na kusimamiwa na Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA). Kushoto ni Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Issa Chikoka na kulia ni Mkurugenzi Mtendaji (MD) wa Mamlaka hiyo, CPA Joyce Msiru akimuelezea RC Hapi maendeleo ya mradi huo.
(Picha na Sauti ya Mara)

Chanzo cha maji cha mradi huo ni Ziwa Vichtoria, na tayari wananchi takriban 5,000 wamenza kupata huduma ya maji safi na salama, baada ya serikali kutoa shilingi zaidi ya milioni 400 kugharimia uhuishaji na usambazaji wa huduma hiyo katika mji mdogo wa Shirati.

MaraOnlineNews-Updates

1 comment:

  1. Safi sana RC Mara,tunaamini Wana Mara watakupa ushirikiano wa kutosha inshallah.

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages