NEWS

Tuesday 13 July 2021

Tarime sasa kumekucha utalii wa ndani, hii siyo ya kukosaAFISA Mhifadhi Mkuu, ambaye pia ni Mkuu wa Kitengo cha Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tutindiga George (mwenye kofia katikati), akizindua ununuzi wa tiketi za safari ya utalii wa ndani, iliyopewa jina la "kuwapokea nyumbu" Serengeti, itakayofanyika Julai 25, 2021 kupitia lango la Lamai lililopo kijiji cha Karakatonga/Gibaso wilayani Tarime, Mara. Anayesaidiana na Mhifadhi Tuti kukata utepe ni Jacob Mugini ambaye ni CEO wa Taasisi ya Mara Online inayoratibu safari hiyo, kwa kushirikiana na Kampuni ya Goldland Hotel Tours. Uzinduzi huo umefanyika leo Julai 13, 2021 katika Hoteli ya Goldland mjini Tarime, ambako tiketi hizo zinapatikana kwa bei nafuu.

MaraOlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages