NEWS

Thursday 29 July 2021

Waziri Aweso anusa ufisadi utekelezaji mradi wa bwawa la maji Maratani, aiagiza TAKUKURU kuuchunguzaWaziri wa Maji, Jumaa Aweso (kulia) alipokwenda kukagua utekelezaji wa mradi wa bwawa la maji la Maratani wilayani Nanyumbu.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso ameiagiza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kuchunguza utekelezaji wa mradi wa bwawa la kuhifadhi maji la Maratani wilayani Nanyumbu, Mtwara ambalo limegharimu shilingi bilioni1.139.

Kufuatia agizo hilo, watumishi wafuatao wametakiwa kufika TAKUKURU: Peter Mdalangwila (Meneja wa RUWASA Uchimbaji-DDCA) na Mhandisi Renard Baseki (aliyekuwa Meneja wa RUWASA Wilaya ya Nanyumbu, kabla ya kuhamishiwa Wilaya ya Newala).

Lengo la wito huo ni kubaini thamani ya fedha iliyotumika na hali halisi iliyoonekana katika mradi ambayo hairidhishi.


Waziri Aweso (katikati waliokaa) katika mkutano na wananchi wilayani Nanyumbu.

Katik ukaguzi huo, Waziri Aweso amekuta umati wa wananchi wakimsubiri na kulalamika kuhusu changamoto kubwa ya maji safi inayowakabili.

Utekelezaji wa ujenzi wa bwawa hilo umefanywa na Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) kupitia Idara ya Uchimbaji-DDCA).

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages