KADA wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)
mkoani Mara, Mwalimu Chacha Heche ameshiriki kupokea chanjo ya UVIKO-19 na
kuwahimiza wafuasi wa chama hicho kujitokeza.
Mwalimu Heche ambaye ni kiongozi wa Mafunzo Chadema
makao makuu amesema kuwa amejitokeza baada ya kushauriana na madaktari wake
wakamhakikishia kwamba chanjo hiyo ni salama hivyo ameitaka serikali itoe elimu
kwa jamii.
“Niko hapa kwa ajili ya kupata chanjo ya korona,
kimsingi nimefanya mawasiliano kwanza na madaktari wangu, watu wa afya
wakanishauri kwamba ni muhimu nikapata hiyo chanjo, kwangu mimi chanjo sio kitu
kigeni nimewahi kupokea chanjo ya homa ya ini na zingine”, amesema Heche.
Heche ambaye amewahi kuwa mwenyekiti wa Chadema mkoa
wa Mara, amewashauri wafuasi wa chama hicho kushiriki kupokea chanjo bila
kujali utofauti za kiitikadi zilizopo kati yao na serikali kwani afya ni jambo
la msingi.
“Pamoja na tofauti yangu ya kiitikadi na serikali
inayoongozwa na Rais Samia Suluhu, kwamba mimi ni kiongozi wa mafunzo Chadema,
lakini kwenye masuala ya msingi kama suala la afya hutakiwi kuleta tofauti
ambazo zinaweza kupotosha watu na kuwachanganya, kwa sababu unamitazamo tofauti
na serikali”, amesema Heche baada ya kupokea chanjo hiyo.
No comments:
Post a Comment