Na Mwandishi Wetu
Watu watano wamekufa baada ya helikopta waliokuwa wakisafiria kuanguka katika MlÃma Kilimanjaro Jumatano jioni.
Helikopta hiyo ni mali ya Kampuni ya KilimediAir Airbus AS350 B3.
Ajali hiyo ilitokea eneo la Barafu juu ya Mlima Kilimanjaro, kwa mujibu wa taarifa ya awali iliyotolewa na Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA).
Taarifa ya Mamlaka ya Safari za Anga Tanzania jana ilithibitisha kutokea kwa ajali hiyo iliyoua watalii wawili kutoka Jamhuri ya Czech, raia wawili wa Tanzania -- muongoza watalii na daktari na rubani wa helikopta raia wa Zimbabwe.
Marekemu hao, kwa mujibu wa TANAPA, wametambuliwa kuwa ni David Plos na Anna Plosova, wote wakiwa na umri wa miaka 30 na raia wa Czech, Watanzania wawili -- Innocent Mbaga -- muongoza watalii -- na Jimmy Daniel -- daktari, na rubani Constantine Mazonde -- raia wa Zimbabwe.
Chanzo cha ajali hiyo bado hakijathibitishwa.

No comments:
Post a Comment