NEWS

Tuesday 24 August 2021

Naibu Waziri Mahundi awasili Manyara kukagua miradi ya majiNAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (pichani juu kushoto), leo Agosti 24, 2021 amewasili wilayani Babati katika mkoa wa Manyara, kwa ziara ya kikazi.

Akiwa wilayani hapo, Mhandisi Mahundi atakagua utekelezaji wa miradi ya maji ya Mayoka-Minjingu na Darakuta-Magugu.


Katibu Tawala wa Mkoa wa Manyara, Caroline Mtapula (kushoto) akifanya utambulisho mbele ya Naibu Waziri Mahundi (kulia). Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Makongoro Nyerere.

Ziara ya Naibu Waziri huyo imekuja siku mbili baada ya Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira Wizara ya Maji, CPA Joyce Msiru kwenda kukagua mradi wa maji wa Darakuta-Magugu katika wilaya ya Babati mkoani Manyara.


CPA Msiru (kulia mbele) alipowasili wilayani Babati kukagua mradi wa maji wa Darakuta-Magugu.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages