NEWS

Monday, 23 August 2021

Professor Mwera Foundation yashiriki kikao kazi cha wadau wa elimu Tanzania




TAASISI ya Professor Mwera Foundation (PMF) imeshiriki kikao kazi cha wadau wa elimu nchini na kutumia fursa hiyo kutambulisha huduma zake za utoaji wa elimu ya msingi, sekondari na chuo.

Kikao hicho kimefanyika jijini Dodoma kwa siku tatu mfululizo (Agosti 16 – 18, 2021), ambapo taasisi ya PMF iliwakilishwa na viongozi kadhaa, akiwemo Meneja wake, Frank Joash.

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais - TAMISEMI, Gerald Mweli (kushoto) na Mkurugenzi wa Elimu Tanzania, Ephraim Simbeye wakipata fulana, kofia na maelezo kuhusu huduma zinazotolewa na PMF - kutoka kwa Meneja wake, Frank Joash (wa pili kulia), wakati wa kikao hicho.


Wadau mbalimbali wa elimu, wakiwemo viongozi kutoka Wizara ya Elimu, wakiwa katika picha ya pamoja jijini Dodoma.


Baadhi ya maafisa elimu wa mikoa wakipata fulana, kofia na maelezo kuhusu huduma zitolewazo na taasisi ya Professor Mwera Foundation, jijini Dodoma.

Hadi sasa PMF inamiliki shule za Mwera Vision English Medium Primary School, Tarime Girls Secondary School na Chuo cha Mafunzo ya Ufundi Stadi - VETA kijulikanacho kwa jina la Tarime Vocational Training College katika mji wa Tarime mkoani Mara.

Mafunzo yanayotolewa katika chuo hicho ni pamoja na ufundi umeme, ushonaji, kompyuta, udereva na magari.


Wadau wa elimu katika picha ya pamoja wakiwa wamevaa fulana na kofia za Professor Mwera Foundation jijini Dodoma

Aidha, taasisi ya PMF inamiliki redio ya kijamii iitwayo Sachita Radio FM na kituo cha Afya cha Sachita, vyote pia vikiwa mjini Tarime.

Mwasisi wa taasisi ya PMF ni Peter Mwera na Mkurugenzi wake ni Hezbon Peter Mwera ambaye pia ni Mwenyekiti wa Wakuu wa Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Kanda ya Ziwa.


Peter Mwera


Hezbon Peter Mwera

(Na Mwandishi wa Mara Online News, Dodoma)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages