NEWS

Saturday 7 August 2021

RC Hapi kukagua miradi ya maendeleo kila wilaya
MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Ally Hapi (pichani juu) anatarajia kuanza ziara ya siku 12 ya kukagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na wananchi na watumishi wa umma katika halmashauri zote tisa za mkoa huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ofisi yake leo Agosti 7, 2021 asubuhi, ziara hiyo itaanzia Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti keshokutwa Jumatatu.

Taarifa hiyo inaonesha kuwa baada ya Serengeti, RC Hapi ataelekea Halmashauri ya Wilaya ya Tarime (Vijijini), kisha Tarime Mji, ikifuatiwa na Rorya, Bunda DC, Bunda Mji, Butiama, Musoma DC na Musoma Manispaa.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages