NEWS

Thursday 12 August 2021

Wanakijiji Nyamakobiti wilayani Serengeti wapata mradi wa maji


MKUU wa Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Dkt Vicent Mashinji jana Agosti 12, 2021 amezindua mradi wa kisima kirefu cha maji katika kijiji cha Nyamakobiti katani Majimoto, uliotekelezwa na Shirika la Life Ministry na wanakijiji.

Diwani wa kata hiyo, Johannes Masirori amesema mradi huo umegharimu shilingi 26,806,000, kati ya hizo, shilingi milioni 26 zimetolewa na shirika hilo na wanakijiji wamechangia nguvu kazi zenye thamani ya shilingi 806,000. "Kisima hiki ni moja ya ahadi zangu," amesema.


DC Dkt Mashinji (kulia) akikata utepe kuzindua kisima hicho. Kushoto ni Diwani Masirori na wengine ni wanakijiji.

Kwa mujibu wa diwani huyo, wananchi 4,311 watanufaika na maji ya kisima hicho, na DC Dkt Mashinji ameahidi kuweka tenki kwa ajili ya kusamba huduma hiyo kwenda maeneo mengine.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages