NEWS

Thursday 9 September 2021

DC Handeni aridhishwa utekelezaji mradi wa maji Mabanda



MKUU wa Wilaya (DC) ya Handeni mkoani Tanga, Siriel Mchembe ameeleza kuridhishwa kwake na maendeleo ya utekelezaji mradi wa maji wa mtaa wa Mabanda.

Utekelezaji wa mradi huo ni agizo lililotolewa na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso mnamo Agosti 26, 2021 ambapo aliwataka watendaji wa wizara hiyo kuhakikisha maji yanafika eneo la Mabanda ndani ya silku 30.


DC Mchembe (mbele) na CPA Joyce Msiru (katikati) wakishiriki utekelezaji wa mradi huo.

“Ninamshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kumtua mama ndoo kichwani, juhudi zake kupitia kwa Waziri Jumaa Aweso zimezaa matunda,” DC Mchembe amesema na kuongeza:

“Ziara [ya Waziri Aweso] aliyoifanya Agosti 26 Handeni, leo tunaona matunda yake, lakini kabla ya yeye kuja alimtuma Katibu Mkuu [wa Wizara ya Maji], Eng Anthony Sanga kujionea hali ilivyo.”


DC Mchembe (kulia mbele) na CPA Msiru (kushoto) katika ziara ya ukaguzi wa mradi huo.

Baada ya Waziri Aweso kukagua vyanzo vya maji na kuwapa watendaji wa wizara hiyo muda wa siku 30 kutatua kero ya maji katika wilaya ya Handeni, Mkurugenzi wa Idara ya Usambazaji Majisafi na Usafi wa Mazingira Wizara ya Maji, CPA Joyce Msiru na timu ya wataalamu waliingia kazini kuanza utetekelezaji wa agizo hilo.

(Na Mwandishi wa Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages