NEWS

Saturday, 17 January 2026

Museveni aibuka mshindi Uchaguzi Mkuu Uganda

Yoweri Kaguta Mseveni

 

Na Mwandishi wetu


Rais Yoweri Kaguta Museveni wa Uganda ameibuka mshindi katika Uchaguzi Mkuu wa nchi hiyo uliofanyika Januari 15, 2026.


Huu ni uchaguzi wa saba kwa rais huyo mkongwe barani Afrika kuwabwaga wapinzani wake katika mfumo wa vyama vingi tangu aingie madarakani na chama chake cha National Resistance Movement mwaka 1986.


Tume ya Uchaguzi ya Uganda imemtangaza Museveni, 81, kwamba amepata kura asilimia 71.6 ya kura zote halali zilizopigwa.


Gwiji huyo wa siasa katika Afrika Mashariki ameiongoza Uganda kwa karibu miongoni minne baada ya kushinda vita ya msituni ya kuzing'oa tawala zilizokuwepo Uganda.


Katika uchaguzi wa Januari 15, 2026, mpinzani wa karibu wa Museveni alikuwa ni Robert Kyagulanyi (Bob Wine), 43, mwanamuziki aliyegeuka kuwa mwanasiasa ambaye kwa chaguzi za hivi karibuni amekuwa akitoa upinzani mkali kwa mkongwe huyo kutoka eneo la Ankole nchini Uganda.


Kwa siasa za Afrika Mashariki, Museveni ndiye Mwalimu wa kutolewa mfano na marais waliopo madarakani  ambao wamemkuta kwenye ulingo wa siasa.


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages