NEWS

Monday, 27 September 2021

Marufuku kubeba silaha maeneo ya starehe Serengeti



SERIKALI wilayani Serengeti imepiga marufuku watu kuingia na silaha, ikiwemo visu katika maeneo ya starehe.

Mkuu wa Wilaya hiyo, Dkt Vicent Mashinji (pichani juu), ametangaza marufuku hiyo Mbele ya Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi aliyekwenda kufungua jengo jipya la Ofisi ya Taifa ya Mashitaka mjini Mugumu, Jumanne iliyopita.

Dkt Mashinji amechukua hatua hiyo baada ya watu kadhaa kuripotiwa kuuawa kwa kuchomwa vizu na kukatwa panga katika maeneo tofauti ya starehe wilayani Serengeti, siku za karibuni.

Akizungumzia suala hilo, Waziri Kabudi amewataka wananchi wanapopandwa hasira kushambulia miti, au kuta kwa ngumi, badala ya binadamu.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages