NEWS

Friday 17 September 2021

Rais Samia ziarani Marekani kuhudhuria Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (pichani juu), leo anaondoka nchini kuelekea New York, Marekani kuhudhuria Mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mwasiliano ya Rais - Ikulu, Jaffar Haniu kwa vyombo vya habari jana, imesema Rais Samia anatarajiwa kuhutubia Baraza hilo Septemba 23, 2021.

"Pamoja na Mkutano huo, Rais Samia pia atahudhuria mikutano ya kilele ya kujadili masuala ya mabadiliko ya tabianchi, usalama wa chakula na utekelezaji wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs)," taarifa hiyo imesema.

Imeongeza kuwa Rais Samia pia anatarajiwa kukutana na Wakuu wa Nchi nyingine na viongozi wa Mashirika ya Kimataifa, kwa lengo la kuimarisha ushirikiano na uhusiano baina ya Tanzania na nchi na taasisi zao.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages