NEWS

Tuesday 28 September 2021

RUWASA yapewa siku 14 kudhibiti upotevu wa maji NjombeNAIBU Waziri wa Maji, Mhandisi Maryprisca Mahundi (pichani juu), ametoa muda wa siku 14 kwa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini na Mijini (RUWASA) kudhibiti upotevu wa maji mkoani Njombe.

Naibu Waziri Mahundi ameelekeza agizo hilo kwa Meneja wa RUWASA Mkoa wa Njombe, Mhandisi Sadick Chakka, akimtaka kuhakikisha tatizo la uvujaji wa maji katika tenki la kijiji cha Usililo wilayani Makete linakoma.

Ametoa agizo hilo Septemba 27, 2021 baada ya kukagua na kubaini tenki hilo linavuja, hali inayosababisha kupungua kwa kiwango cha majisafi yanayotakiwa kuwafikia wananchi.“Meneja wa RUWASA mkoa, hili lipo ndani ya uwezo wako. Nakupa wiki mbili hili tatizo liwe limemalizika. Taarifa inaeleza kuwa kuna upungufu wa maji, halafu hayo yanayopatikana kidogo bado yanavuja. Hili tatizo limalizike haraka,” Naibu Waziri Mahundi amesema.Aidha, Naibu Waziri huyo akiongea na wananchi wa kata ya Luwumbu kijijini Usililo, amewambia Serikali imesikia kilio chao na kutoa fedha kwa ajili ya kuanza kutatua kero ya majisafi katika vijiji vya kata hiyo.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages