NEWS

Monday 13 September 2021

Ugeni mzito Hifadhi ya Taifa Serengeti
MKURUGENZI wa Masuala ya Afrika kutoka Serikali ya Ujerumani, Dkt Stefan Oswald amezuru katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, akiongozwa na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja.

Viongozi hao wamewasili hifadhini hapa leo wakitokea Dar es Salaam kwa ndege, na kupokewa na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi hiyo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Masana Mwishawa na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Dkt Vicent Mashinji.


Mapokezi ya ugeni huo mapema leo asubuhi

Akiwa katika ziara hiyo, Dkt Oswald ataongozwa na Naibu Waziri Mary kukagua maendeleo ya miradi ya uhifadhi inayotekelezwa na Hifadhi ya Serengeti kwa ushirikiano na Shirika la Uhifadhi la Frankfurt Zoological Society (FZS) hifadhini.

Miradi hiyo ni pamoja na karakara ya Seronera, zana za kupambana na ujangili na chumba maalumu cha masuala ya operesheni za hifadhi.

Pia watatembelea Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (WMA) IKONA kuzungumza na viongozi na askari wa hifadhi hiyo.


Mapokezi yakiendelea

Viongozi wengine wanaoshiriki ziara hiyo ni Naibu Kamishna wa Uhifadhi wa TANAPA, William Mwakilema, Kamishna Msaidizi Mwandamizi Idara ya Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa Tanznia (TANAPA), Pascal Shelutete, Mkuu wa Kitengo cha Utalii Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tutindaga George na Meneja Mradi wa FZS Serengeti, Masegeri Rurai.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages