NEWS

Sunday 3 October 2021

Basi la Zakaria, Prado yagongana uso kwa uso, wawili wafa papo hapo
WATU wawili wamefariki dunia papo hapo, baada ya gari walilokuwa wakisafiria kugongana na Zakaria Air Bus uso kwa uso katika kijiji cha Gamasara, nje kidogo ya mji wa Tarime mkoani Mara.

Ajali hiyo imetokea leo Oktoba 3, 2021 - saa 3:15 asubuhi, wakati basi hilo lenye namba za usajili T 906 DLJ likitokea Mwanza na Prado lenye namba T 184 AQT likitokea mjini Tarime.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, waliofariki dunia na miili yao kupelekwa kuhifadhiwa chumba cha maiti katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime, ni ndugu kutoka familia moja ya kijijini Gamasara.

Taarifa zaidi zimeeleza kuwa baadhi ya abiria waliokuwa kwenye basi za Zakaria wamepata majeraha na kuwahishwa hospitalini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Tarime Rorya, ACP William Mkonda amethibitisha kutokea kwa ajili hiyo, vifo vya watu wawili na majeruhi watatu.
"Vifo ni watu wawili na waliojeruhiwa ni watatu ambao tayari wamepelekwa hospitalini kupata matibabu," Kamanda Mkonda ameiambia Mara Online News kwa njia ya simu leo asubuhi.
#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages