NEWS

Thursday 7 October 2021

Facebook: Je ni kwanini wateja wa mtandao huo hawakuweza kupata huduma?


Facebook imeomba msamaha baada ya kushindwa kufanya kazi miongoni mwa wateja wake kote duniani kwa saa kadhaa siku ya Jumatatu.

Programu za WhatsApp na Instagram - ambazo pia zinamilikiwa na kmapuni ya facebook pia zilishindwa kufanya kazi kwa muda huohuo.

Je tatizo lilikuwa lipi?

Kwa ufupi, mifumo ya facebook ilishindwa kuwasiliana na mtandao duniani.

'Ni kama ambaye kuna mtu aliyeaathiri nyaya za kampuni hiyo katika kituo kikuu cha kutoa data na kuzitengenisha na intaneti' , ilielezea kampuni ya miundo msingi ya tovuti CloudFlare.

Maelezo ya facebook yalijaa masuala ya kiufundi.


Ilisema kwamba :"mabadiliko kwenye njia ambazo zinaratibu trafiki ya mtandao kati ya vituo vyetu vya data vimesababisha maswala ambayo yalikatisha mawasiliano haya".

Je ni kwanini wateja wa mtandao huo hawakuweza kupata huduma?

Intaneti hugawanyika kwa mamia ya maelfu ya mitandao. Makampuni makubwa kama Facebook humiliki mitandao yao mikubwa - inayojulikana kama mifumo huru.

Unapotaka kutembelea Facebook au Instagram au WhatsApp, kampyuta yako inatakiwa kujiunga na mtandao wake , kwa kutumia BGP - aina ya huduma ya posta kwa wavuti.

Ili kuweza kuwaunganisha moja kwa moja na wavuti wanaohitaji , BGP hutazama njia zote zilizopo ambazo data zinaweza kutumia kutembea na kutumia njia bora.

Siku ya Jumatatu, facebook ghafla ilisita kutoa habari iliohitajika na mfumo huo ili kufanya kazi.

Ina maana kwamba hakuna hata mtu mmoja aliyekuwa na uwezo wa kuungana na facebook ama mitandao yake mingine.

Je hali hiyo ilikuwa na madhara ya kiwango gani?

Kukatika kwa huduma hiyo kuliathiri vibaya biashara za watu na makampuni kote duniani.

Downdetector, ambayo hufuatilia kukatika kwa huduma hiyo, iliripoti matatizo milioni 10.6 ya kukatika kwa huduma hiyo kote duniani - ikiwa ni idadi kubwa zaidi kuwahi kurekodiwa.

Kwa wengi, kupotea kwa huduma hiyo ulikuwa usumbufu tu. Lakini kwa wafanyabiashara wengine wadogo katika ulimwengu unaoendelea waliokosa njia nyengine za kuaminika kuwasiliana na wateja wao, huenda lilikuwa tatizo kubwa sana.

Vilevile, mashirika mengine ambayo wafanyikazi wake wamekuwa wakifanya kazi mashambani kutokana na mlipuko wa corona wamekuwa wakitegemea WhatsApp kuwasiliana na wenzao.

Je tukio hilo lilifanyikaje?

Ripoti nyingi zilianza kujitokeza mnamo 16: 16 BST Jumatatu kwamba Facebook, Instagram na WhatsApp hazifanyi kazi.

Mwanzoni, hii ilisababisha utani wa kawaida juu ya jinsi watu wataweza kukabiliana, na jibes kutoka kwa wapinzani kama vile Twitter.

Lakini muda mfupi baadaye ikawa wazi kuwa hali hiyo ilikuwa suala kubwa zaidi.

Sheera Frenkel, mwandishi wa teknolojia wa New York Times, aliiambia BBC kwamba ilichukua muda mrefu kurekebisha tatizo hilo kwasababu "watu waliojaribu kutatua tatizo hilo hawakuweza hata kuingia ndani ya jengo" ili kubaini nini kilichosababisha hali hiyo.

''Bado hatujui iwapo tatizo hilo lilitokana na hitilafu ya programu au ni makosa ya kibinadamu''.

Hatahivyo, nadharia kadhaa zimeanza kusambazwa - baadhi wakidai kwamba kuna mtu aliyecheza mchezo mchafu ndani ya kampuni ya Facebook .

Je facebook imelichukuliaje tatizo hilo?

Mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg, baada ya kuona aibu , alilazimika kugeukia mtandao hasimu wa Twitter kuomba msamaha.

Je Facebook imepata hasara ya kiwango gani?

Huenda tatizo kuu kwa Facebook yenyewe ilikuwa athari ambayo ilikuwa nayo kwa mapato na bei za hisa. Kuzima kunamaanisha matangazo hayakutolewa kwa zaidi ya saa sita kwenye majukwaa yake.

Inakadiriwa kwamba, kukatika kwa huduma hiyo huenda kulisababisha hasara ya takriban $6bn (£ 4.4bn) kutoka kwa utajiri wa kibinafsi wa Bwana Zuckerberg, huku hisa zake zikishuka kwa karibu 5%.

Wengine wanakadiria kuwa facebook ilipata hasara ya $ 60m kama mapato.

Vilevile kampuni hiyo imepoteza heshima yake kote duniani.

Chanzo: BBC News

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages