NEWS

Thursday 7 October 2021

Mwanachuo Ualimu Bunda afa kwa kugongwa gari, wenzake 32 wajeruhiwa, dereva mbaroni mwa Polisi
MWANAFUNZI wa Chuo cha Ualimu Bunda, Zuhura, amefariki dunia, huku wenzake 32 wakijeruhiwa kwa kugongwa na gari wakati wakifanya mazoezi ya mchakamchaka.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mara, ACP Longinus Tibishubwamu (pichani juu) amezungumza na Mara Online News kwa njia ya simu na kuthibitisha kutokea kwa ajali hiyo.

Ametaja gari lililosababisha ajali hiyo leo Oktoba 7, 2021 saa 12 asubuhi katika eneo la Manyamanyama, nje kidogo ya mji wa Bunda, kuwa ni lenye namba za usajili T 190 DRB aina ya Nissan Saloon, mali ya Lameck Kisengu, ambaye ndiye alikuwa akiliendesha..

"Gari hilo lilikuwa linatokea Musoma kuelekea Mwanza na tayari tunamshikilia dereva huyo. Majeruhi watano ambao hali zao ni mbaya wamepekwa Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza na wengine wanaendelea kutibiwa na kuruhusiwa," Kamanda Tibishubwamu amesema.

(Na Mwandishi wa Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages