NEWS

Monday 11 October 2021

Rais Samia: Utalii unazidi kuimarika nchini
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan (pichani juu), amesema sekta ya utalii inaendelea kuimarika nchini, baada ya kuyumba kutokana na mlipuko wa janga la UVIKO-19 duniani.

Amesema watalii zaidi ya 490,000 kutoka mataifa mbalimbali wamezuru nchini kati ya Machi na Septemba mwaka huu na anatarajia idadi itaendeleo kuongezeka.

Rais Samia ameyasema hayo katika hotuba yake ya uzinduzi wa Kampeni ya Maendeleo kwa Ustawi wa Taifa na Mapambano dhidi ya UVIKO-19 jijini Dodoma, juzi.Katika hatua nyingine, Mkuu huyo wa nchi ameonya kuwa hatavumilia ubadhirifu wa shilingi trilioni 1.3 zilizotolewa mkopo na Shirika la Fedha Duniani (IMF), kwa ajili ya kugharimia utekelezaji wa kampeni hiyo yenye kaulimbiu inayosema “Pambana na UVIKO-19, Kazi Iendelee”.

“Kwenye fedha hii sitakuwa na huruma na mtu atakayeichezea, kuanzia mawaziri wangu,” Rais Samia amesisitiza.Rais Samia amebainisha kuwa fedha hizo zitaelekezwa katika uboreshaji wa miradi mbalimbali, ikiwemo ya elimu, afya na maji nchini.

Aidha, ameelekeza mamlaka husika kuwapa wakandarasi wa dani kipaumbele katika utoaji zabuni za utekelezaji wa miradi hiyo, huku akionya ukiritimba unaoweza kuichelewesha.“Tuwatumie wakandarasi wenyeji ili fedha hii izunguke hapa nchini,” Rais Samia amesema na kutoa wito kwa sekta binafsi kuchangamkia fursa hiyo kwa kuzalisha bidhaa bora.

(Na Mwandishi wa Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages