NEWS

Thursday 21 October 2021

Tanzania yapata heshima Chuo cha kimataifa cha Maji Uholanzi

Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba
TANZANIA imepata heshima ya kuzungumza katika Chuo maarufu cha Kimataifa cha Maji cha IHE Delft kilichopo Uholanzi (The Netherlands).
Taarifa iliyotolewa jana na kitengo cha Mawasiliano Wizara ya Maji, Imethibithisha kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara hiyo, Mhandisi Nadhifa Kemikimba(pichani juu) atatoa hotuba katika sherehe za ufunguzi wa mwaka wa masomo 2021-2023 leo jioni.

“Mhandisi Kemikimba atatoa hotuba hiyo akiwakilisha Jumuiya ya wananchuo waliosoma IHE Delft”, imesema sehemu ya taarifa hiyo ambayo Mara Online News imepata nakala yake.

Chuo cha IHE Delft kipo chini ya Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na Watanzania wengi wamefanikiwa kupata mafunzo ya viwango vya kimataifa chuoni hapo.

Wanasayansi waliobobea katika sekta ya maji na uhifadhi wa mazingira katika chuo hicho wanauelezea Mto Mara kama mto muhimu unaostahili kutunzwa na kuhifadhiwa kwa manufaa ya kizazi cha sasa na vijavyo.
Mto Mara ni sehemu muhimu ya ikolojia ya Serengeti na una mchango mkubwa katika uhifadhi wa wanyamapori ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ambayo imetunukiwa Tuzo ya Hifadhi Bora zaidi barani Afrika kwa miaka miwili mfululizo (2019 NA 2020).

Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria (LVBWB) inafanya kila linalowezekana kutunza na kuhifadhi Mto Mara kupitia ofisi yake ya Dakio la Mara-Mori lililopo Musoma, huku wadau mbambali zikiwemo jumuiya za watumia maji zikishirikishwa katika jukumu hilo.
Kila mwaka watalii wamekuwa wakimiminika katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kujionea tukio la nyumbu kuvuka Mto Mara kwenda Mbuga ya Maasai - Mara nchini Kenya na kurudi Serengeti.

Mbali na uhifadhi wa ikolojia ya Serengeti - Mara, Bonde la Mto Mara lina mchango mkubwa katika ustawi wa maisha ya watu zaidi ya milioni 1.1 katika nchi za Tanzania na Kenya

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages