NEWS

Tuesday 19 October 2021

‘Tunaahidi kuwa mabalozi wa utalii wa ndani Serengeti’




KUNDI la watalii wa ndani zaidi ya 20 kutoka wilaya ya Tarime mkoani Mara, limetembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na kuahidi kuwa mabalozi wazuri wa utalii wa ndani katika hifadhi hiyo.

“Nimefurahi sana, kila kitu kuanzia mazingira ni ‘amazing’. Tumeona nyumbu wengi, chui na wengine, pundamilia sasa ndio usiseme. Nitakuwa balaozi mzuri,” Mmoja wa watalii hao ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya NMB amesema.


Watalii hao ambao wameingia Hifadhi ya Serengeti kupitia lango la Lamai wiki iliyopita, pia wamepata fursa ya kutembelea mojawapo ya hoteli za kifahari zilizopo katika hifadhi hiyo.

“Thanks a lot, we really had a good time,” Mtalii mwingine ambaye ni mfanyakazi wa Benki ya CRDB amesema.


Baadhi ya watalii wa ndani kutoka Tarime wakifurahia mandhari ya moja ya hoteli za kifahari zilizopo Hifadhi ya Serengeti, huku wakipata kinywaji baridi.

Safari hiyo ya utalii wa ndani iliandaliwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kushirikiana na Kampuni ya Mara Online Safaris, kwa lengo pia la kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere katika kudhimisha Kumbukizi ya Miaka 22 ya Kifo chake, kwani ndiye mwasisi wa utalii nchini.

Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara, Oktoba 18, 2021

1 comment:

  1. Safi sana na hii iwe mfani kwa wengine, tuache kusimiliwa, tusiache wazungu pekeee nasi tunaweza

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages