NEWS

Sunday 24 October 2021

Usafiri wa anga ulivyokwamisha Biashara United mechi ya nchini Libya



TIMU ya Biashara United ya Tanzania, imetaja ukosefu wa usafiri wa ndege kuwa ndiyo uliisababisha kushindwa kwenda nchini Libya kushiriki mechi ya marudio ya Kombe la Shirikisho la CAF.

Mechi hiyo ilipangwa kuchezwa Oktoba 23, mwaka huu kati Biashara United na Al Ahli ya Libya.

Kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Klabu ya Biashara United, Haji Mtete (pichani juu), juhudi za kuisafirisha timu hiyo ziligonga mwamba kwa sababu za kiusalama.

“Mechi ilikuwa inachezwa tarehe 23 na sisi tulipanga kuondoka Dar es salaam kwa kutumia ndege ya kukodi tarehe 21, tulipokea email kuwa route imekuwa cancelled kwa sababu za kiusalama,” Mtete ameimbia Mara Online News kwa njia ya simu, jana Jumapili.

Amesema juhudi za Serikali na TTF kusaidia kupata ndege ya ATCL kwa ajili ya kusafirisha timu hiyo pia ziligonga mwamba, baada ya kukosa vibali vya ndege kwenda Libya kwa wakati mwafaka.

“Ni kweli sisi hatukuwa na pesa lakini kuna taasisi zilikuwa tayari kutulipia kwa njia ya bond,” Mtete amesema wakati akijibu kuhusu uvumi kuwa timu hiyo ambayo imekuwa ikifadhiliwa na kampuni ya Barrick imeshindwa kusafiri kwenda Libya kwa sababu ya ukata wa fedha.

“Mpaka sasa [jana Jumapili jioni] hatujapata official communication (mawasiliano ya kiofisi) kama tutaondolewa, kupigwa faini au mchezo kurudiwa,” amesema.

Amesema pamoja na maandalizi ya muda mrefu kwa ajili ya timu hiyo kusafiri kwenda Libya, tatizo lilitokea mara baada ya ndege za kibiashara zinazoruka na kutua Istambul, Tunusia au Bengazi kufutiwa route kwa kilichoelezwa kuwa ni sababu za kiusalama.

“Commercial flights zote ambazo tulikuwa tutumie route zao kwenda Libya zilifutwa na option ilikuwa kutumia ndege ya kukodi kupitia Juba hadi Bengazi,” amefafanua.

Ndege ya kukodi, Mtete amesema ingegharimu Dola za Kimarekani 75,000.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages