NEWS

Wednesday 13 October 2021

Watalii wa ndani wawasili Hifadhi ya Serengeti kumuenzi Mwalimu NyerereWATALII wa ndani kutoka wilaya ya Tarime mkoani Mara, wakiwa katika picha ya pamoja leo Oktoba 14, 2021 asubuhi, muda mfupi baada ya kuwasili lango la Lamai - tayari kwa kuadhimisha Kumbukizi ya Miaka 22 ya Kifo cha Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, kwa kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.


MKURUGENZI wa Kampuni ya Mara Online Safaris, Jacob Mugini (kushoto mbele) akipokea nyaraka ya malipo ya kiingilio hifadhini kutoka kwa Mhifadhi wa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Watalii wa ndani kutoka Tarime wakiwa katika moja ya hoteli za kifahari hifadhini.

Safari hiyo imeandaliwa na kuratibiwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa kushirikiana na Kampuni ya Mara Online Safaris
.
 
Aidha, safari hiyo ni mwendelezo wa mwitikio wa uhamasishaji kwa wananchi kujitokeza kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, unaofanywa na Blogu ya Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara.


Miongoni mwa wanyamapori waliokuwa kivutio kikubwa kwa watalii hao ni simba wakijipumzisha hifadhini.


#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages