NEWS

Wednesday 6 October 2021

Waziri Aweso ahimiza ushirikiano miradi ya maji




WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso (pichani juu) amewataka wakurugenzi na watendaji wa mamlaka za maji nchini, kuwashirikisha viongozi wa ngazi mbalimbali katika kusimamia utekelezaji wa miradi ya maji nchini.

Waziri Aweso ametoa agizo hilo katika kikoa na wakurugenzi na watendaji hao, kilichofanyika jijini Dodoma leo.



“Ushirikishwaji ni hatua ya msingi ili wananchi wajue na kupata taarifa ya kazi za kuwafikishia huduma ya maji,” amesisitiza.

Amewataka watendaji hao kufanya kazi kwa ubunifu ili kuendelea kuleta mageuzi makubwa katika sekta ya maji.

Akizungumza katika kikao hicho, Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amewataka watendaji hao kuwa na ushirikiano wa dhati katika kufikisha huduma ya maji kwa wananchi.


Mhandisi Sanga

Mhandisi Sanga ametaka juhudi zaidi zielekezwe katika kuboresha miundombinu ili kufikia lengo la utoaji huduma ya majisafi kwa asilimia 85 vijijini na 95 mijini.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages