NEWS

Monday 25 October 2021

Waziri wa Mambo ya Nje Falme za Kiarabu azuru banda la Tanzania DubaiWAZIRI wa Nchi wa Mambo ya Nje wa Umoja wa Falme za Kiarabu, Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan, ametembelea banda la Tanzania kwenye maonesho ya Expo 2020 Dubai.

Afisa Mhifadhi Mkuu na Mkuu wa Kitengo cha Utalii katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti - Tanzania, Tutindaga George (kushoto), akimuonesha Waziri Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan mojawapo ya bidhaa za Tanzania.

Katika ziara yake hiyo aliyoifanya Oktoba 20, 2021, Waziri Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan ameonesha kuvutiwa na sekta ya kilimo na kutaka kufahamu zaidi aina mbalimbali za mazao yanayolimwa nchini Tanzania.

Amevutiwa hasa na kilimo cha maparachichi, ambapo ametaka kujua ni kwa kiasi gani Tanzania imewekeza katika kilimo na uzalishaji wa zao hilo.


Waziri Sheikh Shakhbout bin Nahyan Al Nahyan akizungumza na Mhifadhi Tutindaga.

Waziri huyo ametumia nafasi hiyo pia kuipongeza Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kupata Rais wa kwanza mwanamke, Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Pia, amewapongeza Watanzania kwa kuwa na matumaini makubwa kwa Rais Samia, akisema Tanzania ipo katika mikono salama ya mama wa Taifa, hivyo itaendelea kusonga mbele kiuchumi na kijamii.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages