NEWS

Monday 11 October 2021

Ziara ya Mbunge Ghati, neema Serengeti
MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete (pichani juu kushoto), ameendelea na ziara ya kikazi ya kukagua na kuhamasisha maendeleo ya wananchi.Akiwa wilayani Serengeti leo Oktoba 11, 2021, mbunge ametembelea kituo cha afya Iramba kujionea hali ya utoaji wa huduma na kufahamu changamoto zilizopo.Katika kupunguza changamoto zilizopo, Mbunge Ghati amekabidhi msaada wa shuka kadhaa za kisasa, zenye thamani ya shilingi milioni 1.2, kwa ajili ya wagonjwa wanaolazwa kituoni hapo.


Mbunge Ghati (kushoto) akikabidhi msaada wa shuka.

Baadaye ametembelea Shule ya Sekondari ya Sekondari Kutwa ya Mapinduzi na kuichangia shilingi 800,000 kwa ajili ya mawe tripu tano na mchanga tripu tano.Uongozi wa shule hiyo umetumia nafasi hiyo kumteua Mbunge Ghati kuwa mlezi wa shule hiyo kuanzia leo.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages