NEWS

Monday 29 November 2021

Chuo cha Lindalva Justo chafungua milango MasangaCHUO cha Lindalva Justo Vocational Training Centre kilichopo Masanga wilayani Tarime, Mara, kimefungua milango ya mafunzo ya fani mbalimbali kwa wahitaji wote.

Kwa mujibu wa tangazo la chuo hicho kwenye gazeti la Sauti ya Mara, chuo hicho kitafunguliwa kuanza mwaka wa masomo Januari 12, 2022.

Miongoni mwa fani au kozi zitakazokuwa zinatolewa chuoni hapo ni pamoja na Kiingereza, kompyuata, ushonaji nguo, mapishi mbalimbali na ufundi wa umeme majumbani.

(Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages