NEWS

Friday 19 November 2021

Rorya: Wananchi wamuomba Mbunge Chege asaidie kutatua ugumu wa maisha kwa vijanaWAKAZI wa kijiji cha Ryagoro kilichopo jimbo la Rorya mkoani Mara, wamemuomba Mbunge wao, Jafari Chege kusaidia kutatua changamoto ya ugumu wa maisha kwa vijana.

Wametoa ‘kilio’ hicho mara baada ya Mbunge huyo kusimama kuwasamilia kijijini hapo leo asubuhi.

“Mheshimiwa Mbunge hili suala la ajira kwa vijana ni tatizo kubwa hapa kwetu, angalia namna ya kuboresha vijana,” mmoja wao amesema.

Mbunge Chege (pichani juu kushoto) amejibu hoja hiyo kwa kutoa wito kwa vijana kujiunga kwenye vikundi na kuchangamkia fursa zilizopo, ikiwepo mikopo inayotolewa na halmashauri ya wilaya.

Aidha, Mbunge huyo kijana ameahdi kuwasadia vijana wa Rorya kuwekeza katika kilimo chenye tija, kuanzia Januari mwakani.

(Habari na picha: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages