NEWS

Tuesday 23 November 2021

TAYOHADO yatoa mafunzo kwa watu wenye ulemavu Tarime
SHIRIKA la Afya na Maendeleo ya Vijana Tanzania (TAYOHADO) limeendesha semina ya mafunzo maalumu kwa watu wenye ulemavu katika wilaya ya Tarime mkoani Mara.

Semina hiyo ambayo imefanyika mjini Tarime leo Novemba 23, 2021, imelenga kuelimisha kundi hilo la jamii masuala ya ajira jumuishi, lakini pia kuiwezesha TAYOHADO kutambua changamoto zinazolikabili na kupata mapendekezo ya nini kifanyike ili kuzitatua.


Washiriki wa semina wakifuatilia mada

Mgeni rasmi katika semina hiyo ambaye ni Katibu wa Umoja wa Vijana wa CCM Wilaya ya Tarime (UVCCM), Newton Mwongi ameipongeza TAYOHADO kwa kuona hilo umuhimu wa kuwapatia watu wenye ulemavu mafunzo hayo.

Aidha, Mwongi amewashauri watu wenye ulemavu kuunda vikundi kama hatua ya kujijengea mazingira mazuri ya kupata fursa mbalimbali, ikiwemo mikopo ya fedha kwa za mitaji ya kuanzisha na kuendeleza miradi ya kijasiriamali ili kujikwamua kiuchumi.


Mwongi akizungumza katika semina hiyo

“Undeni vikundi mkaombe mikopo mwanzishe biashara… Serikali yetu imeenda mbali na sasa inatoa mikopo hadi kwa mtu mmoja mmoja.

“Kuna fursa nyingi ndani ya wilaya ya Tarime, kuna mgodi wa dhahabu wa North Mara ambao pia unazalisha fursa za ajira,” Mwongi amesema na kuongeza:

“Lakini pia, kwa ninyi vijana, mjiendeleze kielimu, mtu mwenye ulemavu ukisoma inakuwa rahisi kutatua changamoto za ajira.”


Mratibu wa Mradi, Marwa Mwita (kulia) akizungumza katika semina hiyo. Kulia ni Ofisa Ufuatiliaji na Tathmini, Machera Mkono.

Mwongi aliongeza kwa kusema kuwa atazichukua changamoto hizo na kuziwasilisha kwa viongozi wa juu ili wapate ufumbuzi wa changamoto hizo.

Naye Mwenyekiti wa Shirikisho la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu Tanzania (SHIVYAWATA) Wilaya ya Tarime, Jeremiah Senso amesema waishukuru TAYOHADO kwa mafunzo hayo, huku kuahidi kwenda kuyatumia kwa vitendo.

(Habari na picha: Asteria John, Tarime)

1 comment:

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages