NEWS

Thursday 4 November 2021

Ubovu wa huduma Hospitali ya Tarime: Mwenyekiti wa Kamati ya Afya atishia kuachia ngazi




MWENYEKITI wa Kamati ya Elimu, Afya na Maji katika Halmashauri ya Mji wa Tarime mkoani Mara, Daudi Wangwe (pichani juu), ametishia kujiuzulu wadhifa huo, kutokana na huduma mbovu za Hospitali ya halmashauri hiyo.

Wangwe ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Ketare, ametoa kauli hiyo katika kikao cha baraza la madiwani wa halmashauri hiyo, kilichofanyika ukumbi wa Shule ya Sekondari Tarime, leo Novemba 4, 2021.

“Natamani hata kulia kwa haya yanayoendelea, suala la afya tusilichukulie kama utani.

“Inawezekanaje hospitali ya wilaya inakosa maji, inakosa dawa muhimu na Serikali inaleta dawa, eti huduma ya x-ray haipatikani, chumba cha kuhifadhi maiti hakifanyi kazi, miili inapelekwa Migori (nchini Kenya).

“Kazi yangu ninaipenda, lakini kuliko kupata aibu ni bora nikae pembeni,” Wangwe amekiambia kikao hicho.


Wangwe (aliyesimama) akizungumza kikaoni

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote, amewakumbusha maofisa watendaji wa kata kuongeza umakini wa kuandaa taarifa za kata zao kwa usahihi, ili kuepuka kuwakosesha wananchi wa maeneo yao fursa za maendeleo.

“Ninatoa wito kwa watendaji wa kata, msiandike nyaraka hizi kwa mazoea, muongeze umakini na mtoe taarifa sahihi, sio ku- copy na ku- paste, ili msikoseshe wananchi fursa ya maendeleo,” Komote amesisitiza.


Komote (aliyesisma) akitoa maelekezo kikaoni

Kikao hicho kimeitishwa kwa ajili ya kujadili utekelezji wa miradi ya maendeleo katika kata nane zinazunda halmashauri hiyo.

(Habari na picha zote: Asteria John wa Mara Online News)

2 comments:

  1. Hiyo ya maiti kupelekwa migori sidhani Kama imewahi kutokea

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages