NEWS

Tuesday 30 November 2021

Ujenzi vyumba vya madarasa Tarime Mjini: Viongozi wafanya ziara ya kushtukizaVIONGOZI wa chama tawala - CCM na Serikali wilaya ya Tarime mkoani Mara, leo Novemba 30, 2021 wamefanya ziara ya kushtukiza ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari ya Nyamisangura.

Viongozi hao ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Kanali Michael Mntenjele, Katibu wa CCM Wilaya hiyo, Valentine Maganga na Katibu wa Mbunge Jimbo la Tarime Mjini, Elisha Samo.“Mafundi wetu hawa wasiposhauriwa mara kwa mara, uwezekano wa kujisahau na kujenga chini ya kiwango upo, kwa hiyo niwaombe ninyi wahandisi wetu, endeleeni kukagua hii miradi na kutoa ushauri kwa mafundi,” Maganga amesema.

Aidha, amewatoa wito kwa wananchi kwa ujumla kufuatilia maendeleo ya ujenzi vyumba vya madarasa wilayani na kutoa taarifa kwa mamlaka za juu, pale wanapoona miradi haiendi vizuri.

“Niwaombe wananchi, hii miradi ni ya kwetu na inajengwa kwa fedha ambayo tutailipa, hatujapewa kwa hisani, sio vizuri kuanza kunyoosheana vidole baada ya miradi kukamilika,” amesisitiza.
Kanali Mntenjele (kulia), Maganga (wa pili kushoto) na Samo (wa pili kulia).

Naye Kanali Mntenjele amewataka mafundi wa mradi huo kuwa makini na kuongeza vibarua, ili utekelezaji wake uweze kukamilika kwa wakati na viwango vinavyotakiwa.

(Imeandikwa na Asteria John, Tarime)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages