NEWS

Monday 29 November 2021

Wananchi Serengeti wamshukuru RC Hapi kwa kusaidia kurejesha maji MugumuMWENYEKITI wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, Ayub Mwita Makuruma amemshukuru Mkuu wa Mkoa (RC) wa Mara, Ally Hapi kwa hatua ya kuiamuru TANESCO kurejesha umeme kwenye mitambo ya kusambaza maji katika mji wa Mugumu.

Hivi karibuni, TANESCO iliikatia Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Mugumu (MUGUWASA) huduma ya umeme na kusababisha wakazi wa mji huo kukosa huduma ya maji kwa siku kadhaa mfululizo.


RC Hapi

“Tunamshukuru sana Mhesmhiwa RC wetu kwa kuchukua hatua za haraka kunusuru maisha ya watu wa Mugumu, maana hali ilikuwa ni mbaya,” Makuruma amesema juzi.

Ameongeza “Hata huduma za kitabibu na nyinginezo muhimu zilikuwa hazifanyiki baada ya mji wa Mugumu kukosa maji.”

Makuruma ndiye aliyeibua hoja hiyo katika Kikao cha Ushauri cha Mkoa (RCC) wa Mara, kilichofanyika mjii Musoma chini ya Mwenyeketi wa ambaye ni RC Hapi.


Ayub Mwita Makuruma

Mwenyekiti huyo wa Halmashauri amekieleza kikao hicho kuwa TANESCO ilikata umeme huo kutokana na deni inaloidai MUGUWASA, jambo lililoonekana kumshtua Mkuu huyo wa Mkoa.

“RC aliagiza pale pale kwamba kwanza TANESCO irejeshe umeme ili wananchi wapate huduma ya maji na mambo mengine ya madai wakae mezani, lakini wakati huo wananchi wakiwa wanapata huduma ya maji na hadi sasa maji yapo na hakuna shida,” amesema.

“Kweli tunampongeza sana RC, alifanya kazi nzuri na sisi wananchi wa Serengeti tunamuunga mkono na Mungu aendelee kumjaalia afya njema” Makuruma amesema.

(Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages