NEWS

Sunday 28 November 2021

Maendeleo ya Uhifadhi: TAWA yasema ujangili umepungua Kanda ya Ziwa
VITENDO vya ujangili katika mapori ya akiba yaliyopo Kanda ya Ziwa vimepungua kutokana na juhudi za uhifadhi katika mapori hayo, yakiwemo ya Ikorongo/Grumeti.

“Tuna furaha kuwa hivi sasa tunapata ushirikiano mzuri kutoka kwa wananchi na ujangili unapungua,” Kamanda wa Uhifadhi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA) Kanda ya Ziwa, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi, Laurent Katakweba amesema wilayani Serengeti, hivi karibuni.

Mapori ya akiba ya Ikorongo/Grumeti yapo katika eneo kinga la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, ambayo ni mapito ya wanyamapori, yakiwemo makundi ya nyumbu wanaohama kila mwaka.

Hivyo TAWA inasisitiza kuwa umuhimu wa uhifadhi endelevu wa mapori hayo mawili yenye ukubwa wa kilometa za mraba 993.4 ni mkubwa pia kwa maendeleo ya kiuchumi na kijami.

Mbali na Ikorongo/Grumeti, TAWA Kanda ya Ziwa ina jukumu la kulinda na kuhifadhi mapori ya akiba ya Kijereshi na Maswa.


Kamishna Laurent Katakweba

Pia, TAWA Kanda ya Ziwa inasimamia uhifadhi katika Jumuiya za Hifadhi za Wanyamapori (WMAs) za Ikona (Serengeti) na Makao iliyopo Meatu.

“Tunaomba wananchi kuendelea kutoa ushirikiano na kutoona wanyamapori kama ni maadui, waendelee kuwa walinzi wakuu,” Kamishna Katakweba amesema.

(Chanzo: Gazeti la Sauti ya Mara)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages