NEWS

Wednesday 15 December 2021

Bingwa wa teknolojia kusaidia uzinduzi habari za elimu kwa wasichana

 

Bingwa wa teknolojia duniani kutoka nchini Marekani, Rhonda Vetere ameahidi kusaidia ufadhili wa uzinduzi wa ukurasa maalumu wa habari za elimu kwa wasichana zitakazokuwa zinachapishwa kwenye gazeti la Sauti ya Mara kila Jumatatu.
Rhonda ambaye alishirki katika mbio za Serengeti nchini Tanzania hivi karibuni kuchangisha fedha kwa ajili yakugharimia elimu kwa wasichana, amesema anapenda kuona wasichana wanafikia ndoto zao bila vikwazo.
"Ujumbe wangu mkubwa ni kwamba wasichana wasiache kujifunza maishani, wasome kwa bidii na wasikubali mtu yeyote kukatisha ndoto zao,” Rhonda ameiambia Mara Online News kwa njia ya email kutoka Marekani, wakati akikubali kusaidia juhudi hizo za elimu kwa wasichana.
Uzinduzi huo unatarajiwa kufanyika wiki ijayo mjini Tarime na tayari wadau mbalimbali wa elimu kwa wasichana akiwemo Mkurugenzi wa Shirika la Hope for Girls and Women in Tanzania, Rhobi Samwelly wamethibitisha kushiriki.
Baadhi ya wabunge wa viti maalumu mkoani Mara,  wakiwemo Esther Matiko na Ghati Chomete, nao wameahidi kuunga mkono juhudi hizo ili kuinua elimu kwa watoto wa kike.
Toleo la kwanza la ukurasa huo litachapisha nukuu muhimu za watu maarufu wa kuhamasisha elimu kwa wasichana, ikiwemo mojawapo ya nukuu za Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan zinazosisitiza umuhimu wa watoto wa kike kupewa fursa ya elimu kwa maendeleo ya taifa.
Lengo la ukurasa huo  ni kuongeza msukumo wa jamii kuwekeza kwenye elimu kwa wasichana na kuwawezesha kutimiza ndoto zao za elimu, kwa mujibu wa Mkurugenzi na Mhariri Mtendaji wa gazeti la Suti ya Mara, Jacob Mugini.
“Tunaanza mwaka mpya na zawadi kwa wasichana, tunawashukuru wadau wote waliokubali kutusaidia kuanzisha ukursa wa habari za elimu kwa wasichana, akiwemo bingwa wa tekinolojia  duniani kutoka Marekani, Rhonda Vetere," Mugini amesema leo.
Mugini amesema maandalizi kwa ajili ya hafla hiyo ya uzinduzi yamefikia hatua nzuri.
“Nina furaha kuwakaribisha wadau au mtu yeyote ambaye angependa kuwa sehemu ya mafanikio ya elimu kwa wasichana kujitokeza kutuunga mkono, ili kuimarisha nguvu ya kupiga vita vitendo vinavyokatisha ndoto za elimu kwa watoto wa kike," Mugini ambaye kitalluma ni mwandishi wa habari amasema.

2 comments:

  1. Merry Christmas to All my friends in Uganda and Kenya !
    Dance for Peace and Love Africa.
    Native Americans will be Dancing with You!
    From Sedona, Arizona with Love,
    Victory Dolphin
    Tribal

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages