NEWS

Wednesday 8 December 2021

CRDB wapongezwa kwa kupanda miti 1,000 Serengeti
MKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Ally Hapi leo Desemba 8, 2021 ameipongeza Benki ya CRDB kwa kuunga mkono Serikali katika upandaji miti wilayani Serengeti, wakati wa maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru mkoani Mara.

“Nimepewa taarifa kuwa mmepanda miti 1,000, hongereni sana. Tunawapongeza kwa kazi nzuri ambayo mnafanya kutuunga mkono,” RC Hapi amewamabia wafanyakazi wa Benki ya CRDB, muda mfupi baada ya kushiriki kupanda mmoja wa miti iliyoandaliwa na benki hiyo eneo la Bomani, nje kidogo ya mjini Mugumu, Serengeti.

RC Hapi akipanda mti

Wafanyakazi wa benki hiyo waliongozwa na Meneja wao wa Kanda ya Ziwa, Lusingi Sitta ambaye pia ameshiriki na mwenyeji wake, RC Hapi kupanda miti.


Meneja Sitta (kushoto) akimkabidhi RC Hapi mti kwa ajili ya kupanda

Awali, RC Hapi ameshiriki katika shughuli ya kupanda miti zaidi ya 2,000 katika vijiji vinavyozunguka bwawa la maji la Manchira, ambayo imetolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS).

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages