NEWS

Wednesday 1 December 2021

TANAPA yazungumzia wanyamapori walionasa kwenye tope Hifadhi ya Mikumi



SHIRIKA la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA) limethibitisha tukio la wanyamapori kunasa kwenye tope katika Hifadhi ya Taifa Mikumi.

Taarifa hiyo ya TANAPA imesambazwa kwa vyombo vya habari saa chache, baada ya video fupi kusambaa kwenye mitandao ya jamii leo Desemba 1, 2021 alfajiri, ikionesha wanyamapori wamenasa katika tope hifadhini hapo.


Pascal Shelutete

Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyosainiwa na Meneja Mawasiliano wa TANAPA, Pascal Shelutete, hali hiyo imetokana na ukame uliosababisha upungufu wa maji katika maeneo mbalimbali nchini, yakiwemo ya Hifadhi za Taifa.

“Hata hivyo, mvua zilizonyesha jana jioni tarehe 30.11.2021 zimewezesha maji kiasi kujaa katika mabwawa husika na wanyama kurejea katika hali ya kawaida ya matumizi ya mabwawa,” taarifa hiyo imesema.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages