NEWS

Friday 3 December 2021

Waziri Aweso azindua mradi wa kutumia umeme jua kusukuma maji




WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso leo Desemba 3, 2021 amezindua programu ya kusukuma maji kwa kutumia nishati ya umeme jua katika kijiji cha Zanka wilayani Bahi, Dodoma.

Uzinduzi wa program hiyo yenye thamani ya Dola za Marekani milioni 7.3, ni matokeo ya utafiti uliofanyika mwaka 2015 kuhusu namna ya kutumia nishati ya jua kusukuma maji.

"Teknolojia hii inaenda kupunguza gharama za uendeshaji miradi ya maji, ikiwemo ununuzi wa dizeli,” Waziri Aweso amesema katika hafla hiyo iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Wilaya ya Bahi na wakazi wa eneo hilo.

Waziri Aweso ameainisha kuwa mradi huo unatekelezwa katika mikoa ya Singida, Dodoma, Mtwara, Shinyanga na Tabora.

Mradi huo utanufaisha jumuiya za maji katika vijiji 125, zinazohudumia vijiji 215 vyenye wakazi zaidi ya 560,000 katika wilaya 25.

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages